Machapisho

TASKIU 2021 TUKO MBELE PAMOJA

Picha
HATUTENGANI HATUKAI MBALI, KIDEVU NA NDEVU

TUNAPANDA NGAZI WOTE DAIMA HAKUNA WA KUACHWA NYUMA SIO KWA KABILA DINI JINSIA WALA RANGI WOTE MBELE KWA MBELE

Picha

Taskiu logo

2021 MAY 1 SIKUKUU YA WACHAPA KAZI DUNIANI

Picha
Leo ni siku kubwa leo ni siku ya wale wote wanao Tafuta riziki kwa namna tofauti tofauti wawe maseremala, walimu, madaktari, mafundi ujenzi, makenika na kila aina ya mchapa kazi leo ni siku yetu ila kwa wadau wa TASKIU Leo ni siku yenye kumbukumbu kubwa zaidi kwani ndio siku haki usawa na uchapa kazi viliimarishwa tarehe kama ya leo mwaka mmoja uliopita hivyo kila siku kama hii inapofika wana Taskiu TUnakua kwetu ni siku kubwa zaidi kwa Kuwa siku kama ya leo yani mei mosi tulipata muelekeo mpya katika masuala ya kibiashara kwa kuwapiga chini baadhi ya wadau waliokua wanatumia mali za umoja kinyume na katiba hilo ni jambo kubwa kwa wana taskiu wote popote walipo hivyo tunapenda kuwatakia Sikukuu ya mei mosi siku ya wafanyakazi duniani siku yetu wana taskiu iwabambe kistaili na kazi iendelee

TASKIU LOGO 2021

Picha
Hiyo ndio nembo halisi Ya taskiu grops 2021

HII NI KUBWA KULIKO "WHITE FURNITURE" WAMEKUJA KIVINGINE KABISA KATIKA KARNE HII YA KIDIGITALI WANAKUJIA NA THAMANI ZA KISASA KWA AJILI YA MAJUMBANI NA MAOFISINI

Picha
VIP MDAU MAISHA NI MSWAKI TU SAIVI Neno kinywani mwa wajanja sasa ni WHITE FURNITURE WAkali wa thamani za maofisini na majumbani kutoka Keko Dar Es Salaam wanakuja na bidhaa mpya na za kijanja kinoma noma kama unavyoona hapo pichani ni hatari. woy ni hatari tena wanatisha hawa jamaa ila tena hawajaishia apo ona hizi tena dah, hizo ni meza tu lakini pia makabati wanayo kama ivi ebwanae ni atari umeona na hiyo? cha kufanya bwana ili kujipatia mavitu ya kijanja kama hayo wacheki whatsap namba +255 712 965 608

KWA NIABA YA VIONGOZI WOTE WANACHAMA WOTE NA WASHIRIKA WA TASKIU GROUP TUNAPENDA KUWATAKIA WAISILAMU WOTE MWEZI MWEMA WA TOBA RAMAADHAN TUKUFU

Picha
RAMADHAN KAREEM Wana TASKIU TUmeona sababu kubwa kuwakumbuka wenzetu wanaofunga katika kufanya toba mwezi huu mtukufu wa ramadhan wakiwemo pia wanachama wetu na waislamu wote mwezi huu uwe wa mafanikio tele kwa yale yote mliokusudia pia Msisahau kuliombea taifa letu la TANZANIA katika wakati huu ambapo bado hatujajua hatma kamili itakuaje lakini pia niwakumbushe wanachama wote waislamu maneno ya madam AGNES Jana aliwaomba wanachama wote kuiombea TASKIU Katika mwezi huu mtukufu ili iweze kusonga mbele na kufikia malengo

Kuna haja ya kumpa ofisi bwana Clement Chagu Wadatoga atufanyie mambo makubwa

Picha
CLEMENT CHAGU WADATOGA pichani ndie tumaini la umoja mwaka 2023 kwani kutokana na shinikizo la wadau wa Taskiu Imeonekana wazi viongozi wengi hawatagombea tena nafasi za juu akiwepo mwenyekiti wa sasa Madame Agnes Ambaye ametamka hivi majuzi kuwa ili kuwe na mabadiliko chanya ndani ya umoja wadau wayaone ni afadhali hata uongozi pia ubadilishwe na kutoa wale wote wanaohudumu katika sekta za uongozi zaidi ya miaka 6 lakini pia pendekezo la marekebisho ya katiba 2023 litakalomwezesha mwenyekiti wa umoja kumteua katibu mkuu, mweka hazina na afisa mipango limeonekana kuwa babu kubwa zaidi tofauti na miaka iliyopita watu hawa kuchaguliwa na wanachama lakini swala linalokuja mbele yetu ni swali moja JE KUBADILISHA VIONGOZI WA ZAMANI NA KUWEKA WAPYA NDIO JIBU LA MAFANIKIO? Tunapaswa kujiuliza mara tatu tatu katika maamuzi yetu Ndio maana nikasema kuna haja ya kumpa uenyekiti CLEMENT alafu wengine tukabadilisha ili tupate hekima kwa mkongwe huyu

MOJAWAPO YA PICHA AMBAZO ZINADHIHIRISHA UMAHIRI WA MAFUNDI WETU KATIKA KUIPA DARI YA NYUMBA YAKO MUONEKANO WA KIPEKEE

Picha
ULIMWENGU WETU DUNIA YETU UJUZI WETU +255 710 233 501 KWa maelezo zaidi

HERI YA SIKUKUU YA PASAKA 2021

Picha
KWA niaba ya kamati zote na uongozi wa TASKIU GROUP COMPANY LIMITED tunapenda kuwatakia sikukuu njema

Imetuchukua karibu siku tano wadau wa TASKIU GROUP CO LTD mwanza kuamini kua ni kweli DKT MAGUFULI amefariki

Picha
Huwezi ukamuelezea mazuri ya binafsi tu sisi kama shirika hapana ni pamoja na alivowapenda wanyonge na kuonyesha kuwa yeye ni mtetezi wa wanyonge lipi ambalo unaweza kupinga maneno yake kwani muda wote alimsikiliza mtu yeyote bila kuangalia hali yake hakika tunasema KIMEONDOKA CHUMA LIMEONDOKA JEMBE NGUZO TULOEGEMEA IMEDONDOKA SINA maana kwamba ndio tumedondoka Hapana lakini utakubaliana nami kuyumba tutayumba kidogo yote kwa yote ni kusema tu PUMZIKA BABA TUTAONANA BADAYE

Habari mpya kutoka kamati ya fedha na mipango ni kuwa PASCAL STEVENI amenunua vipande zaidi vya hisa ndani ya kampuni

Picha
Sio kushangaza watu tu bali limeacha nyuso za wanachama wa TASKIU GROUP CO.LTD Katika hali ya burudani na bashasha baada ya kununua tena vipande vya hisa 100 elfu ikiwa ni mwaka mmoja umepita tangu alivyofanya tukio kama hilo Kwa sasa pascal pichani anamiliki hisa elfu 200 zenye thamani ya milioni 150 hiyo ndio safari ya uhakika